Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 130

An-Nisaa 4:130

النساء

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ ٱللَّهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِۦ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ وَٰسِعًا حَكِيمًا

Maana

Na wakitengana, Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja kutoka katika wasaa wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima. [130]

[130] Ikiwa suluhu haikumkinika na ikawa chuki (au karaha) imeshika nguvu zaidi, basi inalazimika kufarikiana. Na wakifarikiana Mwenyezi Mungu atawatosheleza kila mmoja wao kutokana na ukunjufu wa rehema yake na fadhila yake. Na riziki ziko katika mikono ya Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye hikima, na hupanga mambo yote kwa mipango yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ukitokea utengano baina ya mwanamume na mkewe, Allah Mtukufu, Aliyetakasika, atamtosheleza kila mmoja kati yao kwa fadhila Zake na ukunjufu wa neema Zake. Kwani Yeye, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu na Aliyetukuka, ni Mkunjufu wa fadhila na neema, ni Mwingi wa hekima katika hukumu Zake Anazozipitisha kwa waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net