An-Nisaa 4:129
النساءوَلَن تَسْتَطِيعُوٓا۟ أَن تَعْدِلُوا۟ بَيْنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا۟ كُلَّ ٱلْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا
Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wanawake, hata mkikakamia. Kwa hivyo, msiegemee moja kwa moja mkamwacha (mmoja wao) kama aliyetundikwa. Na mkisikizana na mkamcha Mungu, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu. [129]
[129] Kuwafanyia uadilifu wake kwa mapenzi ya daima yasiyo chafuliwa na udanganyifu, na kutendeana usawa katika mapenzi ikawa nipe nikupe, ni jambo lisilo wezekana kuwa. Kadhaalika haiwezi kuwepo usawa katika kuwapenda wake, ikiwa kuna zaidi kuliko mke mmoja. Walakini mkijitahidi, basi msimfanyie ujeuri mmoja wapo, mkamili upande mmoja, na mkamwacha mwengine si mke si mt'alaka. Yapasa mjitengeneze, na muendeshe nyumba zenu kwa wema si kwa ufisadi. Na mcheni Mwenyezi Mungu apate kughufirieni na akurehemuni. Ni shani yake kughufiria na kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hamtaweza, enyi wanaume, kuhakikisha uadilifu kamili wa mapenzi na muelekeo wa moyo kati ya wanawake, namna mtakavyofanya bidii juu ya hilo. Basi msimpe mgongo, yule msiokuwa na haja naye, kabisa kabisa mkamuacha akawa ni kama mwanamke ambaye hana mume wala hakutalikiwa, mkaja mkapata madhambi. Na mkizitengeneza amali zenu mkafanya uadilifu katika ugawaji wenu baina ya wake zenu na mkamcha Allah Mtukufu mkamuogopa juu yao, basi Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net