Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 128

An-Nisaa 4:128

النساء

وَإِنِ ٱمْرَأَةٌ خَافَتْ مِنۢ بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَآ أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَٱلصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ ٱلْأَنفُسُ ٱلشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا

Maana

Na mwanamke akihofia kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na uchoyo. Na mkifanya wema na mkamcha Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. [128]

[128] Na mwanamke akikhofia kuwa mumewe anapuuza mambo ya nyumbani au anayatupa, hayajali, wala hayashughulikii, basi hapana dhambi kwa wote hao wawili kutafuta njia za kusuluhiana kwa mapatano mema na kukurubiana. Na mwenye akili kati yao ni yule anaye anza kutaka masikizano. Na suluhu daima ina kheri, haina shari ndani yake. Linalo zuia masikizano ni kule kuwa kila mmoja kung'ang'ania haki yake kwa ukamilifu, na ugumu na uchoyo wa nafsi unapo wamiliki watu. Wala hapana njia ya kurejeza mapenzi ila mmojapo kati ya wawili kulegeza kamba. Na huyo ndiye mwema, mchamngu, mwenye kujihifadhi na dhulma. Na mwenye kutenda vitendo vyema na akamcha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu anayo khabari ya vitendo vyake, na atamlipa kwavyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwanamke akijua kuwa mumewe ana majivuno na madharau na hashughuliki naye, si makosa kwa wao wawili kusikilizana kwa namna ya kuwaridhisha wao wawili kuhusu kugawa siku na matumizi. Kwani masikilizano ni bora zaidi na ni afadhali zaidi. Na nafsi zimeumbwa zikiwa na tabia ya pupa na ubahili, kama kwamba ubahili upo mbele ya hizo nafsi, hauepukani nazo. Na mkiamiliana na wake wenu vizuri na mkamcha Allah Mtukufu juu yao, basi Allah Mtukufu ni Mjuzi sana wa mnayoyafanya, katika hayo na mengineyo, hakuna kinachofichika Kwake, na Atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net