Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 127

An-Nisaa 4:127

النساء

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِى ٱلنِّسَآءِ ۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِى ٱلْكِتَـٰبِ فِى يَتَـٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّـٰتِى لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلْوِلْدَٰنِ وَأَن تَقُومُوا۟ لِلْيَتَـٰمَىٰ بِٱلْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمًا

Maana

Na wanakuuliza fatwa kuhusiana na wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu anawatolea fatwa juu yao, na yale mnayosomewa katika Kitabu hiki kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi kile walichoandikiwa, na mnapenda kwamba muwaoe, na kuhusu wanyonge katika watoto, na kwamba muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na chochote mnachofanya katika heri, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua. [127]

[127] Watu walimtaka Mtume s.a.w. awambie nini hukumu ya sharia juu ya wanawake. Na wanawake walikuwa, na wangali bado kuwa, ni watu wanyonge. Basi Mwenyezi Mungu amembainishia Nabii wake ili naye abainishe hali ya wanawake, na hali ya wanyonge wengine katika ukoo miongoni mwa watoto na mayatima. Na akataja kuwa mayatima wanawake ambao wanaolewa wala hawachukui mahari yao, na watoto, na mayatima, wote hao watendewe kwa uadilifu na huruma na kuraiwa. Na kwamba kila kheri itendwayo basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua, na Yeye ndiye atakaye ilipa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watu wanakutaka, ewe Nabii, uwaelezee mambo yaliyowatatiza kuyafahamu yanayowahusu wanawake na hukumu zao. Sema, Allah Mtukufu Anawafafanulia kuhusu mambo yao na yale mnayosomewa ndani ya Qur’ani kuhusu mayatima wa kike ambao hamuwapi mafungu yao waliyoandikiwa na Allah Mtukufu ya mahari, mirathi na haki nyiginezo, na mkawa mnapenda kuwaoa au hamuna hamu ya kuwaoa. Na pia Allah Mtukufu Anawafafanulia kuhusu mambo ya madhaifu miongoni mwa watoto na ulazima wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu na kuacha kuwafanyia maonevu kwa kuwanyima haki zao. Na wema wowote mnaoufanya, Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anaujua, hakuna kinachofichika Kwake kuhusu huo na mwingineo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net