An-Nisaa 4:126
النساءوَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ مُّحِيطًا
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika dunia. Na Mwenyezi Mungu amekizingira kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuvizunguka vitu vyote. [126]
[126] Hakika wa kumtakasia niya ni Mwenyezi Mungu, na ndio kwake Yeye inapasa uusilimishe uso wako, yaani umuelekee na umnyenyekee. Huko ndiko kumsafia niya Mwenyezi Mungu aliye umba ulimwengu wote, na ndiye mwenye kuumiliki. Vitu vyote viliomo mbinguni na duniani - nyota, sayari, jua, mwezi, milima, mabonde, majangwa, mashamba n.k. ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kubainikiwa na kila kitu, Mwenye kujua kwa ujuzi mkamilifu wa kuvizunguka vitu vyote avitendavyo mwanaadamu. Na Yeye atamlipa kheri akitenda kheri, na shari akitenda shari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni vya Allah Mtukufu viumbe vyote vilivyoko ulimwenguni. Hivyo ni milki Yake, Aliyetukuka, Peke Yake. Na Allah Mtukufu Amekizunguka kila kitu, hakuna kitu chochote, katika mambo ya waja Wake, chenye kufichika Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net