An-Nisaa 4:125
النساءوَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبْرَٰهِيمَ خَلِيلًا
Na ni nani aliye bora zaidi kwa dini kuliko yule aliyeusilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa ni mwema, na akafuata mila ya Ibrahim mnyoofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwandani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani. [125]
[125] Msingi wa vitendo vyema ni itikadi iliyo sawa. Na bora ya dini ni kumtakasikia niya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ukawa uso wako, na akili yako, na nafsi yako, yote haitaki kitu isipo kuwa kumridhi Mwenyezi Mungu Subhanahu. Kwa hivyo basi ndio fahamu zako zitanyooka sawa kuufahamu ujumbe wa Mitume, na ndio utaweza kushika daima vitendo vilivyo bora, na ukamfuata Baba wa Manabii, Ibrahim a.s. Kwani dini yake Ibrahim ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo Dini inayo elekeza kutaka Haki daima. Na kwa Ibrahim ndiyo umekutana umoja wa Dini, kwa Waislamu, na Mayahudi na Wakristo. Basi ifuateni njia yake. Mwenyezi Mungu hakika amemkirimu Ibrahim, akamwita "Rafiki Mwendani".
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna yoyote aliye mwema wa dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Peke Yake, kwa moyo wake na viungo vyake vyote, hali ya kuwa ni mwema wa maneno na vitendo, mwenye kufuata amri ya Mola wake, akawa amefuata mila ya Ibrãhîm na Sheria aliyoileta na amejiepusha na itikadi mbaya na sheria zilizo batili. Na Allah Mtukufu Alimteua Ibrãhîm, rehema na amani zimshukie, na Akamfanya ni msafiwa Wake miongoni mwa viumbe Wake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya al- khullah (ubui) kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, nao ni daraja ya juu kabisa ya mapenzi na uteuzi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net