An-Nisaa 4:124
النساءوَمَن يَعْمَلْ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَدْخُلُونَ ٱلْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا
Na mwenye kufanya katika mema, akiwa wa kiume au wa kike, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa kiasi cha jicho la kokwa ya tende.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende. [124]
[124] Watendao mema, kwa kadiri ya uwezo wao nao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wataingia kwenye Pepo ya neema, wala hawatapunguziwa hata chembe. Na hapana khitilafu baina ya malipo ya mwanamume na ya mwanamke, kwani mwanamke naye ana waajibu wake, malipo ya vitendo vyema, na adhabu kwa vitendo vibaya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mwenye kufanya matendo mema, awe ni mwanamume au mwanamke, hali ya kuwa anamuamini Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na haki Aliyoiteremsha, basi hao Allah Mtukufu Atawaingiza Peponi, nyumba ya starehe ya daima, na hawatopunguziwa chochote katika thawabu za matendo yao, hata kama ni kadiri ya kitone kilichoko kwenye koko ya tende.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net