An-Nisaa 4:123
النساءلَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَآ أَمَانِىِّ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوٓءًا يُجْزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدْ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا
Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Mwenye kufanya ubaya, atalipwa kwa huo, wala hatajipatia kando na Mwenyezi Mungu mlinzi wala wa kumnusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipo kuwa Mwenyezi Mungu. [123]
[123] Malipo siyo ayatamaniyo mtu na kuyaota bila ya vitendo vyema vizaavyo matunda. Malipo siyo myatamaniyo nyinyi, Waislamu. Wala siyo wayatamaniayo na kuyaota Ahlu-l-Kitabi, Watu wa Biblia, Mayahudi na Wakristo. Bali malipo na kuepukana na adhabu ni kwa Imani na Vitendo Vyema. Atendaye maovu atalipwa kwa vitendo vyake. Wala hampati mlinzi wala wa kumnusuru ila Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Fadhila hizi kubwa hazipatikani kwa matamanio mnayoyatamani, enyi Waislamu, wala kwa matamanio ya Mayahudi na Wanaswara waliopewa Kitabu. Hakika zinapatikana kwa kumuamini Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kikweli na kuyafanya vizuri matendo ya kumridhisha. Na yoyote mwenye kufanya tendo baya, atalipwa kwalo, na hatompata, asiyekuwa Allah Mtukufu, mtegemewa mwenye kusimamia mambo yake wala msaidizi mwenye kumnusuru na kumuepushia adhabu mbaya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net