An-Nisaa 4:122
النساءوَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلًا
Na wale walioamini na wakatenda mema, tutawaingiza katika Bustani zipitazo mito kwa chini yake. Watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo kweli. Na ni nani mkweli zaidi wa kauli kuliko Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio amini na wakatenda mema, tutawaingiza katika Bustani zipitayo mito kati yake. Watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo kweli. Na nani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu. [122]
[122] Huu ndio mwisho wa wafuasi wa Shetani. Ama mwisho wa wafuasi wa Mwenyezi Mungu ni mzuri. Wao ndio walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda mema, wala hawazugwi na mawazo ya uwongo. Hakika Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Mtukufu atawatia katika mabustani yapitayo mito kati yake, chini ya vivuli. Na hayo ni makubwa mno kuliko bustani hizi za duniani. Na hayo ni yakini, kwani ahadi hizo ni ahadi za Mwenyezi Mungu, na ahadi zake haziwi ila ni hakika isiyo geuka, wala haina udanganyifu. Yeye ni mmiliki wa kila kitu. Wala haiwezi kufikirika kuwa yupo yeyote yule aliye mkweli kwa neno lake na ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliokuwa wakweli katika kumuamini kwao Allah Mtukufu, Aliyetukuku, na wakafuatanisha Imani yao na matendo mema, basi Allah Mtukufu Atawaingiza, kwa ukarimu Wake, ndani ya mabustani ya Pepo ambayo chini ya majumba yake ya fahari na miti yake inapita mito, hali ya kukaa milele humo. Hiyo ni ahadi inayotoka kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ambaye Haendi kinyume na ahadi Yake. Na hapana yoyote aliye mkweli zaidi, katika neno lake na ahadi yake, kuliko Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net