Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 121

An-Nisaa 4:121

النساء

أُو۟لَـٰٓئِكَ مَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا

Maana

Hao makao yao ni Jahannam, na wala hawatapata makimbilio kutoka humo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao makao yao ni Jahannamu, na wala hawapati makimbilio kutoka humo. [121]

[121] Hakika hao walio zipoteza akili zao na wakafuata wasiwasi wa Shetani anao watia katika nafsi zao, mwisho wao ni kuendea Jahannamu, wala hawatapata njia ya kutoka huko.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao marejeo yao ni Jahanamu; na hawatapata mapenyo wala mahali pa kukimbilia ili kuepukana nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net