Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 120

An-Nisaa 4:120

النساء

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ إِلَّا غُرُورًا

Maana

Anawaahidi, na anawatia tamaa. Na Shetani hawaahidi isipokuwa udanganyifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet'ani hawaahidi ila udanganyifu. [120]

[120] Shetani huwapambia shari, wakaiona nzuri, na huwaahidi manufaa watayo pata pindi wakitenda kitendo fulani, na huwatia katika nafsi zao matumaini ya kuyatumai. Na hapana lolote analo waahidi na analo wapambia ila ni udanganyifu mtupu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Shetani anawaahidi wafuasi wake ahadi za urongo na anawavutia kwa matamanio ya urongo yenye udanganyifu; ahadi zake kwao hazikuwa isipokuwa ni udanganyifu usio na ukweli wala dalili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net