An-Nisaa 4:143
النساءمُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلًا
Wanayumbayumba baina ya huku na huko. Huku hawako na huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, kabisa hutompatia njia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako na huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, kabisa hutompatia njia. [143]
[143] Na hawa wanaafiki ni watu wanao taradadi, wanababaika. Kwenu hawapo, na kwao makafiri hawapo katika kila hali. Na hayo ni kwa sababu ya udhaifu wa imani, na udhaifu wa nafsi, na kwa sababu ya kupotoka na Haki. Na mwenye kuandikiwa kupotoka na Mwenyezi Mungu tangu hapo azali, basi huna njia wewe ya kumwongoa sawa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hali ya hawa wanafiki ni kutokuwa na msimamo, kuchangayikiwa na kubabaika, hawathibiti kwenye hali moja, hawako pamoja na Waumini wala hawako pamoja na makafiri. Na yoyote ambaye Allah Mtukufu Ameupotoa moyo wake usimuamini na usishikamane na uongofu Wake, huyo hutampatia njia ya kufikia uongofu na yakini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net