Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 144

An-Nisaa 4:144

النساء

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلْكَـٰفِرِينَ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا۟ لِلَّهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَـٰنًا مُّبِينًا

Maana

Enyi mlioamini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio wasaidizi wandani badala ya Waumini. Je, mnataka kumfanyia Mwenyezi Mungu hoja iliyo wazi juu yenu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?. [144]

[144] Hakika katika sababu za unaafiki ni kuwa wanaafiki wamewafanya watu wasio kuwa Waumini kuwa ndio walinzi wao, marafiki zao, watawala wao, na ndio wa kuwanusuru. Enyi Waumini! Yaacheni haya, muepukane nayo. Wala msiwafanye makafiri ndio wa kukunusuruni, wakukutawalini, mkawanyenyekea. Na hapana shaka yoyote mkifanya hivyo mnampa Mwenyezi Mungu hoja iliyo wazi ya kukuhojini. Mtakuja ingia pamoja na wanaafiki, na mtadhalilika. Kwani inakuwa hamfanyi utukufu wenu utoke kwa Mwenyezi Mungu, na kwa haki, na vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake! Msiwapende na kuwategemea wenye kukanusha Dini ya Allah Mtukufu na mkaacha kuwategemea Waumini na kuwapenda. Je, mnataka kwa kuwapenda maadui wenu kumpa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, hoja iliyo wazi kuwa nyinyi si wakweli katika Imani yenu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net