An-Nisaa 4:145
النساءإِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ فِى ٱلدَّرْكِ ٱلْأَسْفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا
Hakika, wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika Moto, wala hutampata yeyote wa kuwanusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru. [145]
[145] Hakika wanaafiki kwa sababu ya unaafiki wao watakuwa katika vina vya Jahannamu. Wao wako chini kabisa huko, na daraja ya mwisho kabisa. Wala hutompata wa kuwanusuru, wa kuwatetea na adhabu hiyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wanafiki watakuwa kwenye mahandaki ya chini kwa chini ya Moto Siku ya Kiyama. Na hutawapatia wao, ewe Mtume, yoyote wa kuwaokoa atakayewakinga wao wasifikie mwisho huu mbaya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net