Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 146

An-Nisaa 4:146

النساء

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ وَأَصْلَحُوا۟ وَٱعْتَصَمُوا۟ بِٱللَّهِ وَأَخْلَصُوا۟ دِينَهُمْ لِلَّهِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ ٱللَّهُ ٱلْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا

Maana

Isipokuwa wale waliotubu, na wakatengenea, na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake Dini yao, basi hao wako pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atawapa Waumini ujira mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Isipo kuwa wale walio tubu, na wakatengeneza na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakamtakasia Dini yao Mwenyezi Mungu. Basi hao ni pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atakuja wapa Waumini ujira mkubwa. [146]

[146] Isipo kuwa wale katika wao walio tubia, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakaungana naye Yeye peke yake, na wakajitakasa, na wakaelekeza nyuso zao kwake, na wakatenda mema. Wakifanya haya basi ndio wanakuwa miongoni mwa Waumini. Watapata malipo ya Waumini. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha waahidi Waumini malipo makubwa duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Isipokuwa wale ambao walirejea kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, wakatubia Kwake, wakazirekebisha hali zao zilizoharibika za ndani na za nje, wakawategemea waja Wake Waumini, wakashikamana na dini ya Allah Mtukufu na wakamtakasia Yeye, Aliyetakasika kutokana na kila sifa ya upungufu. Hao ni pamoja na Waumini duniani na Akhera; na Allah Mtukufu Atawapa Waumini malipo makubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net