Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 147

An-Nisaa 4:147

النساء

مَّا يَفْعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمْ إِن شَكَرْتُمْ وَءَامَنتُمْ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمًا

Maana

Mwenyezi Mungu atafanyia nini kuwaadhibu ikiwa mtashukuru na mkaamini? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushukuru, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu hakuadhibuni mkimshukuru na mkamuamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea shukrani na ndiye Mwenye kujua. [147]

[147] Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hana alitakalo kwenu ila mumuamini Yeye, na muishukuru neema yake. Mkiwa hivyo basi hampati adhabu, bali mtapata malipo ya kheri na shukrani. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kushukuria waja wake kwa vitendo vyema, na ni Mjuzi, anajua hali zao zote njema na mbaya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu hatawapa adhabu iwapo nyinyi mumefanya amali njema na mumemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake. Kwani Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Hana haja na yoyote asiyekuwa Yeye. Yeye Atawaadhibu waja kwa makosa yao. Allah Mtukufu ni Mwenye kuwarudishia shukrani(1) waja Wake kwa utiifu wao Kwake, ni Mjuzi wa kila kitu. 1 Maana ya Shãkir ikinasibishwa na Allah Mtukufu machache». Ang. Tafsiri ya Ibn Kathîr Sura:2, aya

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net