An-Nisaa 4:148
النساءلَّا يُحِبُّ ٱللَّهُ ٱلْجَهْرَ بِٱلسُّوٓءِ مِنَ ٱلْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا
Mwenyezi Mungu hapendi kutajwa mabaya hadharani isipokuwa kwa aliyedhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
MWENYEZI MUNGU hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. [148]
[148] Mwenyezi Mungu anawakataza waja wake wasiseme maneno maovu, ila yule aliye patwa na dhulma. Ni halali kwake kumshitaki aliye mdhulumu, na autaje uovu aliyo tendewa. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kusikia vyema maneno ya aliye dhulumiwa. Na ni Mjuzi wa dhulma ya mwenye kudhulumu. Na atamlipa kwa kitendo chake hicho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapendi Allah Mtukufu kwa yoyote adhihirishe neno ovu. Lakini yaruhusiwa kwa aliyedhulumiwa amtaje aliyemdhulumu kwa uovu alionao, ili akibainishe alichodhulumiwa nacho. Na daima Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia mnayoyadhihirisha na ni Mwenye kuyajua mnayoyaficha kati ya hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net