Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 149

An-Nisaa 4:149

النساء

إِن تُبْدُوا۟ خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا۟ عَن سُوٓءٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا

Maana

Mkidhihirisha wema au mkiuficha, au mkiyasamehe mabaya, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Muweza mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mkidhihirisha wema au mkiuficha, au mkiyasamehe maovu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Muweza. [149]

[149] Mkiyadhihirisha mema myatendayo, au mkayaficha, au mkamsamehe anaye kufanyieni uovu, Mwenyezi Mungu atakulipeni kwa kufuata khulka yake Mtukufu, ya kusamehe na hali ana uwezo kaamili. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni mwingi mno wa kusamehe, Mwenye kukamilika uwezo wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Amehimiza Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwamba watu wasamehe, na Akaweka msingi wa jambo hilo kwa Muumini, ima aidhihirishe kheri au aifiche. Na vilevile katika kukosewa, ima adhihirishe kuwa amekosewa katika hali ya kutafuta haki yake kwa aliyemkosea au asamehe na apuuze. Na kusamehe ni bora. Kwani miongoni mwa sifa za Allah Mtukufu ni kuwasamehe waja Wake pamoja na uwezo Wake juu yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net