An-Nisaa 4:150
النساءإِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا۟ بَيْنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا۟ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا
Hakika, wale wanaomkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanasema: 'Wengine tunawaamini na wengine tunawakufuru.' Na wanataka kushika njia iliyo kati ya hayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya. [150]
[150] Hakika wasio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanao taka kufanya ubaguzi katika imani ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanasema: Tunawaamini baadhi ya Mitume, sio wote, hao wanawaamini wawapendao na wanawakataa wasio wapenda. Na lilio waajibu ni kuwaamini wote, kwani Imani haikubali kukatwa mapande mapande.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wanaomkanusha Allah Mtukufu na Mitume Wake, kati ya Mayahudi na Wanaswara, na kutaka kutenganisha baina ya Allah Mtukufu na Mitume Wake, kwa kumuamini kwao Allah Mtukufu na kuwakanusha Mitume Wake Aliowatuma kwa viumbe Wake, au wautambue ukweli wa baadhi ya Mitume na kuacha kuwatambua wengine na wadai kwamba baadhi yao wamemzulia Mola wao urongo na wanataka kujifanyia njia ya kuelekea kwenye upotofu waliouanzisha na uzushi waliouzua.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net