Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 115

An-Nisaa 4:115

النساء

وَمَن يُشَاقِقِ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ ٱلْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ ٱلْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِۦ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِۦ جَهَنَّمَ ۖ وَسَآءَتْ مَصِيرًا

Maana

Na mwenye kumpinga Mtume baada ya kubainikiwa na uongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini, tutamuelekeza alikoelekea, na tutamuingiza katika Jahannam. Na hayo ni marejeo maovu zaidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu. [115]

[115] Na anaye mpinga Mtume s.a.w. baada ya kwisha itambua Njia ya Haki na Uwongofu, na akaifuata njia isiyo kuwa ya Waumini, na akaingia kwenye urafiki na maadui wa Waumini, basi huyo atakuwa na hao. Kwani amekhiari kuwa hao ndio wawe marafiki zake na walinzi wake. Mwenyezi Mungu atakuja mtia Motoni Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kuenda kinyume na Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye baada ya kubainikiwa na haki na akafuata njia isiyokuwa njia ya Waumini na haki ambayo wako nayo, basi tutamuacha na muelekeo wake, hatutamuongoza kwenye heri na tutamtia ndani ya Moto wa Jahanamu, akiteseka kwa joto lake. Ni mabaya yaliyoje marejeo haya kuwa ndio mwisho wa mtu!

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net