An-Nisaa 4:114
النساءلَّا خَيْرَ فِى كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَىٰهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَـٰحٍۭ بَيْنَ ٱلنَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِ ٱللَّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا
Hakuna heri katika mengi ya wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujira mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa. [114]
[114] Hakika wale wanao kaa wakipanga mambo yao kisirisiri, mambo hayo hayana kheri, kwa sababu shari ndio huchipuka katika ufichoni. Lakini ikiwa mazungumzo hayo ni kwa jambo la sadaka ya kuwapa watu, au kufanya jambo lolote lisio baya, au kupanga mipango ya kusuluhisha baina ya watu, hayo si mabaya. Kwani hayo ni mambo ya kheri. Na mwenye kufanya hivyo kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Subhanahu Wataa'la, basi Mwenyezi Mungu atampa malipo makubwa duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna manufaa katika mengi ya maneno ya watu ya siri baina yao, isipokuwa yawapo ni mazungumzo yenye kuita kwenye kufanya mema ya utoaji sadaka au maneno mazuri au kuleta upatanishi baina ya watu. Na mwenye kuyafanya mambo hayo, kwa kutaka radhi ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, akitarajia thawabu Zake, tutampa thawabu nyingi zilizo kunjufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net