Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 113

An-Nisaa 4:113

النساء

وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكَ وَرَحْمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٌ مِّنْهُمْ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمْ ۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَىْءٍ ۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚ وَكَانَ فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا

Maana

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao lingedhamiria kukupoteza. Na hawapotezi isipokuwa nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima, na akakufundisha yale uliyokuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao linge dhamiria kukupoteza. Wala hawapotezi ila nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hikima na amekufundisha uliyo kuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa. [113]

[113] Lau kuwa Mwenyezi Mungu hakukufadhili kwa kukuteremshia Wahyi, Ufunuo, na akakupa rehema ya kutambua na kufahamu hakika, kikundi cha wapotovu kingependa kukupoteza. Lakini hawapotezi ila nafsi zao. Kwani Mwenyezi Mungu ni muangalizi wako, na ndiye mwenye kukuonyesha haki. Hayakufikilii madhara ya mipango yao na upotezi wao. Yeye Mwenyezi Mungu amekuteremshia Qur'ani Tukufu ambayo hiyo ndiyo mizani ya haki, na ameutuza moyo wako kwa hikima, na amekufundisha Sharia na hukumu ambazo ulikuwa hukuzijua ila kwa kufunuliwa na Yeye. Hakika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yako daima ni kubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau si Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kukuneemesha, ewe Mtume, kukurehemu kwa neema ya unabii na kukuhifadhi, kwa taufiki Yake, kwa wahyi Aliokuletea, wangaliazimia watu, miongoni mwa wale wanaozifanyia hiana nafsi zao, kukupotosha na njia ya haki. Na wao kwa kufanya hivyo, huwa hawampotoshi yoyote isipokuwa nafsi zao. Na hawawezi kukudhuru kwa kuwa Allah Mtukufu Amekuhifadhi, Amekuteremshia Qur’ani na Sunnah yenye kuifafanua, na Amekuongoza ukajua elimu ambayo hukuwa ukiijua hapo nyuma. Na fadhila za Allah Mtukufu Alizokuhusisha nazo ni jambo kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net