An-Nisaa 4:112
النساءوَمَن يَكْسِبْ خَطِيٓـَٔةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِۦ بَرِيٓـًٔا فَقَدِ ٱحْتَمَلَ بُهْتَـٰنًا وَإِثْمًا مُّبِينًا
Na mwenye kuchuma kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika kashfa na dhambi iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na atendaye kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika dhulma na dhambi iliyo wazi. [112]
[112] Na mwenye kutenda makosa na madhambi kisha akamsingizia mwenginewe asiye na kosa alilo litenda - kama vile mwizi kaiba kitu kisha akamsingizia wizi mtu mwengine - mtu huyo ana dhambi mbili. Moja ni uwongo na uzushi, na la pili lile kosa lilio wazi la kuiba.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mwenye kufanya kosa bila kukusudia au akatenda dhambi kwa kukusudia kisha akamsingizia, yale aliyoyafanya, mtu asiye na hatia, atakuwa amebeba urongo na dhambi zilizo wazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net