An-Nisaa 4:111
النساءوَمَن يَكْسِبْ إِثْمًا فَإِنَّمَا يَكْسِبُهُۥ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا
Na mwenye kuchuma dhambi, basi ameichumia nafsi yake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na anaye chuma dhambi, basi ameichumia nafsi yake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima. [111]
[111] Hakika madhara ya madhambi ni juu ya yule yule ayatendayo. Mwenye kuchuma madhambi basi anajidhuru mwenyewe. Na alitendalo linamuangukia mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na kutukuka anajua aliyo yatenda, na atamchukulia kwa mujibu wa hikima yake. Atamuadhibu au atamsamehe kwa mujibu wa hikima yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Mwenye kufanya dhambi kwa kusudi, hakika huwa akijidhuru nafsi yake peke yake. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni Mjuzi wa uhakika wa mambo ya waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika hukumu Zake Azitowazo kwa waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net