Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 110

An-Nisaa 4:110

النساء

وَمَن يَعْمَلْ سُوٓءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُۥ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورًا رَّحِيمًا

Maana

Na anayetenda uovu au akaidhulumu nafsi yake, kisha akaomba kufutiwa dhambi kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. [110]

[110] Mlango wa toba, hakika, uwazi. Anaye tenda kitendo kiovu cho chote, au akajidhulumu nafsi yake kwa kufanya maasi, kisha akamtaka msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu, atamkuta Mwenyezi Mungu yu tayari kukubali toba yake, na kumghufiria madhambi yake. Kwani ndio mwendo wake Mwenyezi Mungu kughufiria na kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kufanya tendo baya au akajidhulumu nafsi yake kwa kufanya mambo yaliyo kinyume na hukumu ya Allah Mtukufu na sheria Yake, kisha akarudi kwa Allah Mtukufu kwa kujuta kwa aliyoyafanya akitaraji Amsamehe na dhambi zake Amsitirie, basi atamkuta Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha na ni mwingi wa huruma kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net