Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 109

An-Nisaa 4:109

النساء

هَـٰٓأَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ جَـٰدَلْتُمْ عَنْهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فَمَن يُجَـٰدِلُ ٱللَّهَ عَنْهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا

Maana

Hivi ni nyinyi hawa mmewabishania katika uhai huu wa duniani. Basi ni nani atakayewabishania dhidi ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hivyo nyinyi mmewatetea hawa katika uhai huu wa duniani. Basi nani atakaye watetea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea?. [109]

[109] Ikiwa nyinyi mnawatetea hao wakosa wasipate adhabu ya duniani, basi hatopatikana wa kuwatetea Siku ya Kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu na kukubali kuwa ni mlinzi wao wa kuwasaidia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haya nyinyi, enyi Waumini, mnatoa hoja za kuwatetea hawa mahaini wa nafsi zao katika huu uhai wa kilimwengu. Basi, ni nani mwenye kumhoji Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa kuwatetea wao Siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa? Au ni nani atakayekuwa wakili wao Siku ya Kiyama?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net