An-Nisaa 4:108
النساءيَسْتَخْفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ ٱلْقَوْلِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا
Wanawaficha watu, wala hawamfichi Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapopanga njama usiku kwa maneno asiyoyapenda. Na Mwenyezi Mungu ameyazingira vyema wanayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanataka kujificha kwa watu, wala hawataki kujificha kwa Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapo panga njama usiku kwa maneno asiyo yapenda. Na Mwenyezi Mungu anayajua vyema wanayo yatenda. [108]
[108] Wanajificha, na wanataka kujisitiri kwa watu wasiione khiana yao. Wala hayumkini kuzificha khiana zao kwa Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye daima yu pamoja nao. Na wao usiku usiku hukubaliana kwa maneno yasiyo mridhi Mwenyezi Mungu ya kuwasingizia tuhuma watu wasio na makosa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua vyema, na hapana kitu kinacho weza kujificha na ujuzi wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wao wanajificha na watu ili wasipate kuyaona matendo yao mabaya, wala hawajifichi na Allah Mtukufu wala hawamuonei haya, ilhali Yeye, Mtukufu wa mambo, Yupo na wao kwa ujuzi Wake, Anawaona wanapopanga, kipindi cha usiku, maneno Asiyoridhika nayo. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ameyazunguka(kwa ujuzi wake) maneno yao yote na vitendo vyao vyote, hakuna kitu chochote chenye kufichika Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net