Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 107

An-Nisaa 4:107

النساء

وَلَا تُجَـٰدِلْ عَنِ ٱلَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا

Maana

Wala usiwabishanie wale wanaozihini nafsi zao. Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi yule ambaye ni haini mkubwa, mwenye dhambi nyingi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala usiwatetee wanao khini nafsi zao. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi aliye khaaini, mwenye dhambi. [107]

[107] Wala usiwatetee wale wanao fanya khiana, na wakaendelea mno katika kuificha hiyo khiana katika nafsi zao. Kwani Mwenyezi Mungu hampendi ambaye mtindo wake ni khiana na kufanya madhambi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usiwatetee wanaozifanyia hiana nafsi zao kwa kumuasi Allah Mtukufu. Hakika Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa za upungufu, Hampendi yule ambaye hiana yake imekuwa kubwa na dhambi zake zimekuwa nyingi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net