An-Nisaa 4:106
النساءوَٱسْتَغْفِرِ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا
Na omba Mwenyezi Mungu kufutiwa dhambi. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. [106]
[106] Na unapo hukumu baina ya watu muelekee Mwenyezi Mungu, na ukumbuke utukufu wake, na uombe maghfira yake na rehema yake. Kwani kughufiria na kurehemu ndio shani yake Subhanahu wa Taa'la.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na utake msamaha kwa Allah Mtukufu katika hali zako zote. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe kwa wanaotarajia nyongeza za mema Yake na vipewa vya msamaha Wake, ni Mwingi wa huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net