An-Nisaa 4:105
النساءإِنَّآ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ ٱلنَّاسِ بِمَآ أَرَىٰكَ ٱللَّهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَآئِنِينَ خَصِيمًا
Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa kile alichokuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa mahaini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa makhaaini. [105]
[105] Tumekuteremshia hii Qur'ani kwa haki na kwa kweli. Imekusanya kila lilio la haki. Inabainisha haki mpaka Siku ya Kiyama, ili iwe ni taa yako ya kukupa mwangaza kuwahukumu watu. Basi hukumu baina yao, wala usiwepiganie walio makhaaini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tumekuteremshia Qur’ani, ewe Muhammad, iliyokusanya haki, ili utoe uamuzi baina ya watu wote kwa wahyi ambao Allah Mtukufu Amekuletea na Akakufahamisha. Basi usiwe ni mwenye kuwatetea wale wanaozifanyia hiana nafsi zao, kwa kuificha haki, kwa kuwa wamekudhihirishia maneno yaliyo kinyume na ukweli.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net