An-Nisaa 4:104
النساءوَلَا تَهِنُوا۟ فِى ٱبْتِغَآءِ ٱلْقَوْمِ ۖ إِن تَكُونُوا۟ تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ ۖ وَتَرْجُونَ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا يَرْجُونَ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا
Wala msilegee katika kuwafukuzia kaumu hawa (ya maadui). Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyoumia. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu yale wasiyoyataraji. Na hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima. [104]
[104] Msilegee kuwafukuzia makafiri walio kwisha kukutangazieni vita na wanajaribu kukushambulieni kila pahala. Hakika vita havikosi maumivu. Ikiwa nyinyi Waumini mmepata majaraha na mengineyo, na wao makafiri pia wameyapata machungu. Khitilafu yenu ni kuwa wao hawapiganii Haki, wala hawataraji kitu kwa Mwenyezi Mungu; na nyinyi mnataka Haki na mnataraji radhi za Mwenyezi Mungu na neema za kudumu. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu na vyao, naye ni Mwenye hikima, anamlipa kila mtu kwa alitendalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msiwe walegevu katika kuwatafuta maadui wenu na kupigana nao. Mkiwa mnahisi uchungu wa vita na matokeo yake, basi maadui wenu pia wanahisi uchungu wake zaidi, na pamoja na hivyo, hawakomi kupigana nanyi. Basi nyinyi ni aula kwa hilo kuliko wao, kwa kuwa nyinyi mnatarajia thawabu, nusura na kupewa nguvu, na wao hawatarajii hayo. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa hali zenu zote, ni Mwenye hekima katika maamrisho Yake na uendeshaji mambo Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net