An-Nisaa 4:103
النساءفَإِذَا قَضَيْتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ قِيَـٰمًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا ٱطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ ۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتْ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ كِتَـٰبًا مَّوْقُوتًا
Na mkishamaliza Swala, basi mtajeni Mwenyezi Mungu hali ya kuwa mmesimama, na mkikaa, na kwa mbavu zenu. Na mtakapotulia, basi simamisheni Swala. Kwani, hakika Swala juu ya Waumini ni andiko lililowekewa nyakati maalumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala. Na mtapo tulia basi shikeni Sala kama dasturi. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu. [103]
[103] Na mkisha Swala ya vita, inayo itwa Swala ya Khofu, msisahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu daima. Mkumbukeni nanyi mmesimama, mnapigana, mmekaa, na mmelala. Kwani kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kunatia nguvu nyoyo, na kuzituliza. Khofu ikiondoka pakawa na utulivu basi timizeni Swala kwa ukamilifu, kwani Swala imefaridhiwa juu ya Waumini isaliwe kwa nyakati zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mtakapomaliza Swala, endeleeni kumtaja Allah Mtukufu katika hali zenu zote. Na hali ya woga iondokapo, itekelezeni Swala kikamilifu, wala msiifanyie dharau, kwani Swala ni faradhi katika nyakati zijulikanazo katika Sheria.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net