Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 116

An-Nisaa 4:116

النساء

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِۦ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًا

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi kwa hakika amepotea upotovu wa mbali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali. [116]

[116] Hakika mwisho huu wa kuumiza ni wao hao vile vile, kwani hao ni maadui wa Uislamu. Mfano wake ni mfano wa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Hakika kila dhambi yaweza kughufiriwa, ila kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kumuabudu mwenginewe asiye kuwa Yeye, na kumpinga Mtume katika Haki. Ni shani ya Mwenyezi Mungu kusamehe madhambi, ila dhambi ya kumshirikisha Yeye katika ibada. Kwa jenginelo lisilo kuwa hili Yeye humsamehe amtakaye. Anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada na kumtegemea, basi huyo ameipotea Haki, na amekuwa mbali nayo mno; kwani mtu huyo ameifisidi akili yake na nafsi yake pia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Hasamehe Akishirikishwa na Anasamehe madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwenye kumfanyia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Aliye Mmoja, Aliye Pekee, mshirika yoyote, miongoni mwa waja Wake, atakuwa yuko mbali sana na haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net