Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 4 · Aya ya 117

An-Nisaa 4:117

النساء

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ إِنَـٰثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَـٰنًا مَّرِيدًا

Maana

Wao hawawaombi badala yake Yeye isipokuwa vya kike, na wala hawamuombi isipokuwa Shetani aliyeasi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shet'ani aliye asi. [117]

[117] Katika upotovu ulio wazi kabisa ambao uko mbali na Haki ni ule wa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Huyo anaabudu kitu ambacho hakisikii wala hakioni, hakidhuru wala hakinafiishi. Na huita hiyo miungu yake kwa majina ya kike, kama Laata na Uzza na Manaata na mengineyo ya majina ya kike. Yeye hakika kwa hivyo anamuabudu Shetani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Vile wanavyoviabudu washirikina badala ya Allah Mtukufu si chochote isipokuwa ni masanamu yasiyonufaisha wala kudhuru, na hawaabudu isipokuwa Shetani aliyemuasi Allah Mtukufu aliyefikia kiasi kikubwa cha kuharibika na kuharibu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nisaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net