An-Nisaa 4:118
النساءلَّعَنَهُ ٱللَّهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا
Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shetani akasema: Hakika, nitachukua sehemu maalumu katika waja wako.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako. [118]
[118] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha mfukuza huyu Shetani kutokana na kivuli cha rehema yake, na amemjaalia awe katika njia ya upotovu. Na Shetani ameapa, na amejichukulia ahadi mwenyewe, kuwa atachota miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu idadi maalumu awapumbaze kwa upotovu wake na awatie wasiwasi kwa shari yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Alimfukuza kwenye rehema Yake. Na Shetani Akasema, «Nitalichukua fungu maalumu la waja wako niwapoteze kimaneno na kivitendo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net