Az-Zumar 39:16
الزمرلَهُم مِّن فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِّنَ ٱلنَّارِ وَمِن تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ ۚ ذَٰلِكَ يُخَوِّفُ ٱللَّهُ بِهِۦ عِبَادَهُۥ ۚ يَـٰعِبَادِ فَٱتَّقُونِ
Yatawekwa juu yao matabaka ya moto, na chini yao matabaka. Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yatawekwa juu yao mat'abaka ya moto, na chini yao mat'abaka. Kwa hayo Mwenyezi Mungu anawakhofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi! [16]
[16] Hawa walio khasirika watakuwa na mat'abaka ya Moto yalio rindikwa juu yao, na chini yao hali kadhaalika. Kwa namna ya adhabu hiyo ndio Mwenyezi Mungu anawahadharisha waja wake. Enyi waja wangu! Basi yaogopeni mateso yangu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao wenye kupata hasara watawekewa juu yao siku ya Kiyama, wakiwa ndani ya Jahanamu, vipande vya adhabu juu yao vinavyotokana na Moto, kana kwamba ni sakafu zilizojengewa na pia chini yao. Adhabu hiyo yenye sifa hizo ndio ile ambayo Mweyezi Mungu anawaogopesha nayo waja Wake ili wajihadhari nayo. Hivyo basi, enyi waja wangu, niogopeni kwa kuzifuata amri zangu na kujiepusha na matendo ya kuniasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net