Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 15

Az-Zumar 39:15

الزمر

فَٱعْبُدُوا۟ مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِۦ ۗ قُلْ إِنَّ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْخُسْرَانُ ٱلْمُبِينُ

Maana

Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Sema: Hakika waliohasirika ni wale waliojihasiri na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Sema: Hakika walio khasirika ni wale walio jikhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo khasara iliyo dhaahiri. [15]

[15] Ewe Muhammad! Waambie: Ninamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na ibada yangu haina shirki wala riya. Na nyinyi ikiwa mnaijua Njia yangu nanyi hamnit'ii, basi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Waambie: Hakika wenye kupata khasara ni wale walio jitupa kwa upotovu wao wenyewe, na wakawatupa ahali zao kwa kuwapoteza wao Siku ya Kiyama. Ama hakika kupotoka huko ndio khasara iliyo timia na iliyo dhaahiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi nyinyi, enyi washirikina, abuduni mnachotaka badala ya Allah Mtukufu miongoni mwa mizimu na masanamu na visivyokuwa hivyo katika viumbe Vyake, kwani hilo halinidhuru mimi chochote. Na hili ni onyo na tahadharisho kwa anayemuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu na akamshirikisha mwingine pamoja na Yeye. Sema, ewe Mtume, «Hakika wale wenye hasara kikweli ni wale waliopata hasara ya nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama.» Na hiyo ni kwa sababu ya kuwapoteza duniani na kuwapotosha na njia ya Imani. Jua utanabahi kwamba hawa washirikina kupata hasara ya nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama ndiko kupata hasara kuliko wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net