Az-Zumar 39:14
الزمرقُلِ ٱللَّهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُۥ دِينِى
Sema: Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu. [14]
[14] Ewe Muhammad! Waambie: Ninamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na ibada yangu haina shirki wala riya. Na nyinyi ikiwa mnaijua Njia yangu nanyi hamnit'ii, basi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Waambie: Hakika wenye kupata khasara ni wale walio jitupa kwa upotovu wao wenyewe, na wakawatupa ahali zao kwa kuwapoteza wao Siku ya Kiyama. Ama hakika kupotoka huko ndio khasara iliyo timia na iliyo dhaahiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, «Kwa hakika Mimi ninamuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika, nikimtakasia ibada yangu na utiifu wangu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net