Az-Zumar
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
لَهُم مِّن فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِّنَ ٱلنَّارِ وَمِن تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ ۚ ذَٰلِكَ يُخَوِّفُ ٱللَّهُ بِهِۦ عِبَادَهُۥ ۚ يَـٰعِبَادِ فَٱتَّقُونِ 16
{16} Kisha akataja ukubwa wa mashaka yatakayowapata, akasema: "Yatawekwa juu yao matabaka ya moto na chini yao matabaka." Kwa hayo tuliyoielezea, adhabu ya wakazi wa Motoni ni mjeledi ambao kwa huo Mwenyezi Mungu anawachungia waja wake kwenda kwenye rehema zake na "Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake. Enyi waja wangu! Nicheni Mimi," na ni karipio kutokana na yale ambayo yanawasababishia adhabu. Ametakasika Yule ambaye amewarehemu waja wake katika kila jambo! Pia amewasahilishia njia zinazofikisha huko na akawahimiza kuzifuata. Akawatia moyo kwa kila kitu ambacho nafsi inatamani sana, na nyoyo zinatulia juu yake. Akawatahadharisha tahadharisho kubwa sana dhidi ya kufanyia kazi mambo yasiyokuwa hilo na akawatajia sababu za kuwakataza hadi wayaache.