Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 17

Az-Zumar 39:17

الزمر

وَٱلَّذِينَ ٱجْتَنَبُوا۟ ٱلطَّـٰغُوتَ أَن يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ لَهُمُ ٱلْبُشْرَىٰ ۚ فَبَشِّرْ عِبَادِ

Maana

Na wale wanaojiepusha ibada potovu, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao jiepusha na ibada potovu, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu. [17]

[17] Na wale wanao jitenga na masanamu na mashet'ani wasiyakurubie, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote, wanayo bishara tukufu katika mwahala mote. Basi Ewe Muhammad! Wape bishara nzuri waja wangu wanao sikiliza kauli na wakaifuata iliyo bora na yenye kuwaongoa kwendea katika Haki. Hao tu, si wenginewe, ndio Mwenyezi Mungu atao wafikisha kwenye Uwongofu. Na hao tu, si wenginewe, ndio wenye akili zilizo nawirika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliojiepusha kumtii Shetani na kuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu na wakatubia kwa Allah Mtukufu kwa kumuabudu na kumtakasia Dini, basi hao wana bishara njema duniani ya kutajwa vyema na kuafikiwa na Allah Mtukufu, na bishara njema huko Akhera ya kupata radhi za Allah Mtukufu na starehe za daima Peponi. Basi wape habari njema, ewe Nabii, waja wangu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net