Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 39 · Aya ya 18

Az-Zumar 39:18

الزمر

ٱلَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ ٱلْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُۥٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَىٰهُمُ ٱللَّهُ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمْ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ

Maana

Ambao husikiliza maneno, wakafuata lililo bora yake. Hao ndio aliowaongoa Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambao husikiliza maneno, wakafuata lilio bora yao. Hao ndio alio waongoa Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili. [18]

[18] Na wale wanao jitenga na masanamu na mashet'ani wasiyakurubie, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote, wanayo bishara tukufu katika mwahala mote. Basi Ewe Muhammad! Wape bishara nzuri waja wangu wanao sikiliza kauli na wakaifuata iliyo bora na yenye kuwaongoa kwendea katika Haki. Hao tu, si wenginewe, ndio Mwenyezi Mungu atao wafikisha kwenye Uwongofu. Na hao tu, si wenginewe, ndio wenye akili zilizo nawirika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ambao wanasikiliza maneno na kufuata yaliyo sawa zaidi. Na maneno mazuri zaidi na yaliyo sawa zaidi ni maneno ya Allah Mtukufu kisha ni maneno ya Mtume Wake. Hao ndio wale ambao Allah Mtukufu Amewaafikia kwenye usawa na haki na akawaongoza kwenye tabia na matendo bora zaidi; hao ndio watu wenye akili zilizotimia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zumar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net