Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 8

Faatir 35:8

فاطر

أَفَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ فَرَءَاهُ حَسَنًا ۖ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ ۖ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَٰتٍ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا يَصْنَعُونَ

Maana

Je, yule aliyepambiwa matendo yake mabaya na akayaona ni mema - basi hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa amtakaye. Basi, nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Yule aliye pambiwa a'mali zake mbaya na akaziona ni njema - basi hakika Mwenyezi Mungu humwacha akapotea amtakaye, na humwongoa amtakaye. Basi nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anajua wanayo yafanya. [8]

[8] Wamekuwa hawatambui? Je! Yule ambaye Shetani kampambia vitendo vyake viovu na mwenyewe akaona ni vizuri, ni kama aliye hidika kwa uwongofu wa Mwenyezi Mungu na akaliona jema kuwa ni jema, na uovu akauona kuwa ni uovu? Kwani hakika Mwenyezi Mungu humwacha akapotea amtakaye katika wanao khiari njia ya upotovu, wakaiona ndiyo njia ya kuifuata. Na humhidi amtakaye miongoni mwa walio ikhiari njia ya hidaya kuwa ndiyo njia ya kuifuata. Basi usiihiliki nafsi yako kwa kuwasikitikia wapotovu na kuwaonea huruma. Hakika Mwenyezi Mungu anajua uovu wautendao, naye atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, yule ambaye Shetani anampambia matendo yake maovu ya kumuasi Allah Mtukufu, kukufuru na kuwaabudu wasiyekuwa Yeye miongoni mwa waungu na masanamu, akayaona ni mazuri yenye kupendeza, (Je, yeye) ni kama yule ambaye Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Amemuongoza akaliona zuri kuwa ni zuri na ovu kuwa ni ovu? Hakika Allah Mtukufu Anampoteza Anayemtaka na Anamuongoza Anayemtaka. Basi usijiangamize kwa kuwa na huzuni juu ya ukanushaji wa hawa waliopotea. Hakika Allah Mtukufu Anayajua maovu yao na Atawalipa kwa hayo malipo mabaya kabisa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net