Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 9

Faatir 35:9

فاطر

وَٱللَّهُ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ ٱلرِّيَـٰحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَسُقْنَـٰهُ إِلَىٰ بَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَحْيَيْنَا بِهِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ كَذَٰلِكَ ٱلنُّشُورُ

Maana

Na Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndivyo kama hivyo kutakavyokuwa kufufuliwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma Pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyo kufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndivyo kama hivyo kutakavyo kuwa kufufuliwa. [9]

[9] Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anaye zituma pepo ziyatimue mawingu yaliyo rindika kwa mvuke wa maji. Tena tukayasukuma hayo mawingu mpaka kwenye nchi yenye ukame, tukaihuisha ardhi yake baada ya kuwa ilikuwa imekufa. Kama tunavyo itoa mimea katika ardhi, basi hali kadhaalika tutawatoa maiti makaburini Siku ya Kiyama. Rejea maoni ya ki-ilimu juu ya Aya 57 katika Surat Al Aa'raaf.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Ndiye Ambaye Anapeleka upepo, ukatikisa mawingu, tukayaongoza hadi pale kwenye ardhi kavu, hapo mvua ikateremka, tukahuisha kwa mvua hiyo ardhi baada ya ukavu wake, na hapo mimea ikawa rangi ya kijani. Mfano wa kuhuisha huko, Allah Mtukufu Atawahuisha wafu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net