Faatir 35:10
فاطرمَن كَانَ يُرِيدُ ٱلْعِزَّةَ فَلِلَّهِ ٱلْعِزَّةُ جَمِيعًا ۚ إِلَيْهِ يَصْعَدُ ٱلْكَلِمُ ٱلطَّيِّبُ وَٱلْعَمَلُ ٱلصَّـٰلِحُ يَرْفَعُهُۥ ۚ وَٱلَّذِينَ يَمْكُرُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَمَكْرُ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُوَ يَبُورُ
Mwenye kutaka utukufu, basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye hupanda neno zuri, na tendo jema Yeye hulitukuza. Na wanaopanga vitimbi vya maovu, watapata adhabu kali. Na vitimbi vyao vitaondokea patupu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye hupanda neno zuri, na a'mali njema Yeye huitukuza. Na wanao panga vitimbi vya maovu watapata adhabu kali. Na vitimbi vya hao vitaondokea patupu. [10]
[10] Mwenye kutaka utukufu na nguvu na akazitafute kwa kumt'ii Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye ndiye Mwenye nguvu zote. Kumwendea Yeye ndio linapanda neno jema. Na Mwenyezi Mungu huinyanyua a'mali njema na akaipokea. Na wale wanao wapangia Waumini vitimbi vya kuwadhuru watapata adhabu iliyo kali. Na hizo njama zao zitafisidika, hazito leta hayo waliyo yakusudia, wala hazileti natija yoyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yoyote yule atakaye utukufu duniani au Akhera, basi autake kutoka kwa Allah Mtukufu, na hilo halipatikani isipokuwa kwa kumtii Yeye, kwani utukufu ni wa Allah Mtukufu. Na mwenye kujitukuza na kiumbe, Allah Mtukufu Atamdhalilisha; na Mwenye kumtukuza Muumba, Allah Mtukufu Atamtukuza. Kwake Yeye utajo wake utapanda, na tendo jema Analiinua juu. Na wale wenye kutenda mabaya watapewa adhabu kali. Na vitimbi vyao vitaangamia na vitaharibika na havitawafaidisha kitu chochote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net