Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 11

Faatir 35:11

فاطر

وَٱللَّهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَٰجًا ۚ وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِۦ ۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِۦٓ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ

Maana

Na Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akawafanya mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, isipokuwa kwa elimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, isipokuwa yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akakufanyeni mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, ila kwa ilimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, ila yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu. [11]

[11] Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na udongo. Kwani ndivyo hivyo alivyo muumba baba yenu Adam. Kisha akakuumbeni kutokana na tone ya manii, nayo ni maji yanayo miminwa katika tumbo la uzazi, nayo pia ni katika chakula kinacho toka kwenye udongo. Kisha akakufanyeni waume na wake. Wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai ila kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Wala hauongezwi umri wa mtu yeyote, wala haupunguzwi ila husajiliwa katika Kitabu. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali, mepesi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Alimuumba baba yenu Ᾱdam kwa mchanga kisha Akajaalia kizazi chake kitokane na maji dhalili, kisha Akawafanya nyinyi wanaume na wanawake. Na hakuna mwanamke yoyote anayeshika mimba wala anayezaa isipokuwa Analijua hilo. Na hakuna mtu anayepewa maisha marefu au umri wake ukapunguzwa isipokuwa hayo yamo ndani ya Kitabu kilichoko Kwake, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa, kabla mama yake hajashika mimba yake na kabla hajamzaa. Hayo yote Allah Mtukufu Ameyadhibiti na ameyajua kabla hajamuumba, hayataongezwa yale aliyoandikiwa wala hayatapunguzwa. Hakika kule kuwaumba nyinyi, kuzijua hali zenu na kuziandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa ni jambo rahisi na sahali kwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net