Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 7

Faatir 35:7

فاطر

ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ

Maana

Wale waliokufuru watakuwa na adhabu kali; na wale walioamini na wakatenda mema watapata msamaha na ujira mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio kufuru watakuwa na adhabu kali; na walio amini na wakatenda mema watapata msamaha na ujira mkubwa. [7]

[7] Wanao mkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake watapata adhabu kali. Na wanao muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wakatenda mema watapewa kutokana na Mwenyezi Mungu kusamehewa madhambi yao, na ujira mkubwa kwa vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale waliokataa kwamba Allah Mtukufu, Yeye Peke Yake, Ndiye Mola wa kweli, na wakakataa kile walichokuja nacho Mitume Wake, watakuwa na adhabu kali huko Akhera. Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, watapata msamaha kutoka kwa Mola wao na kufutiwa dhambi zao baada ya kuzifanya zisitirike, na watakuwa na malipo mema makubwa, nayo ni Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net