Faatir 35:44
فاطرأَوَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَكَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعْجِزَهُۥ مِن شَىْءٍ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا
Je, hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinachoweza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye uweza wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uweza. [44]
[44] Je! hao hukaa na wakakanya tu ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina, bila ya wao kusafiri katika ulimwengu wakaangalia kwa macho yao athari za maangamizo yaliyo wateremkia walio kuwa kabla yao kwa sababu ya kuwakadhibisha kwao Mitume? Na kabla ya wao yalikuwako mataifa yaliyo kuwa na nguvu kushinda wao. Nguvu zao hazikuweza kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye hashindwi na chochote kilioko mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye ilimu kubwa kabisa, Mwenye uweza mkubwa kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, hawatembei makafiri wa Makkah kwenye ardhi, wakaona ulikuwa vipi mwisho wa wale waliokuwa kabla yao, kama vile ‛Ᾱd, Thamūd na mfano wao, na yale yaliyowapata ya maangamivu na yaliyowapata majumba yao ya uharibifu walipowakanusha Mitume, na makafiri hao walikuwa ni wakali zaidi na ni wenye nguvu zaidi kuliko makafiri wa Makkah? Na hakuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na kitu chochote mbinguni wala ardhini chenye kumlemea na kumpita. Hakika Yeye ni Mjuzi sana wa matendo yao, ni Mwenye uwezo wa kuwaangamiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net