Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 43

Faatir 35:43

فاطر

ٱسْتِكْبَارًا فِى ٱلْأَرْضِ وَمَكْرَ ٱلسَّيِّئِ ۚ وَلَا يَحِيقُ ٱلْمَكْرُ ٱلسَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِۦ ۚ فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ ٱلْأَوَّلِينَ ۚ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ ٱللَّهِ تَبْدِيلًا ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ ٱللَّهِ تَحْوِيلًا

Maana

Kwa kutakabari kwao katika nchi, na kufanya vitimbi vya uovu. Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliyevifanya. Hebu, hawangojei yale yaliowasibu watu wa kale? Basi hutapata mabadiliko katika mtindo wa Mwenyezi Mungu. Wala hutapata mageuko katika mtindo wa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa kutakabari kwao katika nchi, na kufanya vitimbi vya uovu. Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya. Hebu hawangojei yalio wasibu watu wa kale? Basi hutapata mabadiliko katika mtindo wa Mwenyezi Mungu. Wala hutapata mageuko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu. [43]

[43] Wameikimbia Haki kwa kupandwa na kiburi katika nchi, na kuona ari kumnyenyeka Mtume na Dini aliyo kuja nayo. Wakapanga njama za vitimbi viovu. Na ni Shetani ndiye aliye waongoza hata wakaiacha Dini na wakaingia kumpiga vita Mtume. Na wala madhara ya vitimbivi viovu hayampati mtu ila yule yule aliye vipanga. Basi watu hao wanangojea nini isipo kuwa sunna ya Mwenyezi Mungu iliyo wasibu wale walio watangulia? Basi hutoipata njia ya Mwenyezi Mungu anavyo yafanyia mataifa ibadilike, kama wanavyo tumai hawa wapangaji vitimbi yawe kinyume na walio watangulia. Na kabisa hutopata mwendo wa Mwenyezi Mungu ubadilishe njia ulio elekea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kuapa kwao si kwa nia nzuri na kutafuta haki, isipokuwa huko ni kuwafanyia viumbe kiburi katika ardhi, wanakusudia kwa huko kuapa kufanya vitimbi vibaya, udanganyifu na ubatilifu. Na vitimbi vibaya haviwashukii isipokuwa wenyewe. Basi hawana lolote la kungojea, hao wenye kiburi na wenye vitimbi, isipokuwa ile adhabu iliyowashukia waliokuwa kama wao ambao waliwatangulia, Hutaupatia mpango wa Allah Mtukufu mabadiliko wala kugeuka. Hakuna yoyote anayeweza kubadilisha wala kujiepusha na adhabu yeye mwenyewe wala mwingine.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net