Faatir 35:42
فاطروَأَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ لَئِن جَآءَهُمْ نَذِيرٌ لَّيَكُونُنَّ أَهْدَىٰ مِنْ إِحْدَى ٱلْأُمَمِ ۖ فَلَمَّا جَآءَهُمْ نَذِيرٌ مَّا زَادَهُمْ إِلَّا نُفُورًا
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kuapa kwao, kwamba akiwajia mwonyaji, bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote. Lakini alipowajia mwonyaji, hakuwazidishia ila kuikimbia hiyo Haki.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kuapa kwao, kwamba akiwajia mwonyaji bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote. Lakini alipo wajia mwonyaji hakuwazidishia ila kuikimbia hiyo Haki, [42]
[42] Na makafiri waliapa kwa jina la Mwenyezi Mungu mwisho wa juhudi yao kutilia nguvu kiapo chao, ya kwamba bila ya shaka akiwajia Mtume kuwaonya basi wao hapana shaka watakuwa miongoni mwa mataifa walio ongoka zaidi kuliko hao wenginewe walio wakadhibisha Mitume wao. Lakini alipo wajia Mtume kutokana na wao wenyewe, akiwaonya, hakuwazidishia kwa kuwaonya kwake na kuwanasihi, isipo kuwa kuikimbia Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakanushaji wa kikureishi waliapa kwa Allah Mtukufu viapo vikali kwamba wakijiwa na mtume kutoka kwa Allah Mtukufu wa kuwaonya mateso ya Allah Mtukufu, watakuwa ni wenye kusimama wima zaidi na wenye kufuata haki zaidi kuliko Mayahudi, Wanaswara na wengineo. Na alipowajia Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), hilo halikuwaongezea wao isipokuwa kuwa mbali na haki na kuikimbia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net