Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 41

Faatir 35:41

فاطر

إِنَّ ٱللَّهَ يُمْسِكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَآ إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayezuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipo kuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe. [41]

[41] Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuia mpango wa mbingu na ardhi usivurugike, na ndiye anaye zihifadhi mbingu na ardhi zisiondoke. Na lau akizijaalia kuondoka hapana wa kuweza kuzihifadhi hizo isipo kuwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Hakika Yeye ni Mpole, hafanyi papara kuwaadhibu wakhalifu. Yeye ni Msamehevu wa madhambi ya wenye kurejea kwake wakatubu. Aya hii tukufu inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la peke yake ndiye Muumba mbingu na ardhi. Yeye ndiye Mwenye kuzishika zisiondoke. Kwani hivi vitu viliomo mbinguni vya karibu na mbali vinavyo onekana katika qubba la mbingu vimeshikamana kwa mujibu wa mpango maalumu wa namna ya pekee alio uumba Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Kutukuka. Na Yeye ndiye aliye viwekea mvutano usio katika kwa kupita zama na vizazi, na ndiye anaye vihifadhi visikosee mizani yao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ndiye Mwenye uweza huu, wala hapana mwenginewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Anazizuia mbingu na ardhi zisiondoke pale zilipo. Na lau zitaondoka pale zilipo, hakuna yoyote baada Yake Atakayezizuia. Allah Mtukufu ni Mpole katika kuahirisha mateso kwa makafiri na waasi, ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia dhambi zake na akarudi Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net